WANAZI WA SIMBA 'WAMPA' SALUTE DOGO WA LUHANGWA

DOGO muokota mipira katika Uwanja wa Soka wa Majaliwa uliopo Luhangwa mkoani Lindi, amewashika wanazi wa klabu ya Simba kwa namna alivyoonekana kutaka mabingwa hao watetezi waibuke na ushindi katika mechi yao dhidi ya Namungo.
Dogo huyo aliyekuwa
nyuma ya lango la Namungo, mara kwa mara alionekana akirudisha mipira haraka
ilipotoka upande wake ili kuzuia ucheleweshwaji wa muda na wakati John Bocco
alipofunga bao lake la pili, uzalendo ulimshinda kiasi cha kujikuta
akishangilia kwa nguvu.
Na hata bao la tatu
lililofungwa na Morisson, almanusura aingie uwanjani kushangilia.

Post a Comment