MWANAUME USITONGOZE KILA MWANAMKE ALIYE KARIBU, WENGINE WAMEWEPO MARAFIKI TU

KATIKA pitapita zangu, nimeikuta hii article mahali, nikaamini ni somo zuri kwa wasomaji wangu. Nimeiweka kama nilivyoikuta....
"Kipindi nasoma, naishi home
kwa wazee, mfanyakazi wa ndani aligundulika ana mimba. Ikabidi ahojiwe muhusika
ni nani. Ile nyumba watoto wa kiume tulikuwa watano ( kuna mtoto wa baba mdogo
nae alikuja kutembea maana alikuwa likizo chuo).
"Kulingana na mazingira ya
pale home, sio rahisi yule dada kutembea na mtu wa nje ya nyumba, kwahiyo ilo
swala lilimpa mzee hasira sana, maana ilikuwa wazi muhusika wa ile mimba ni
kati ya sisi watano.
"Kikao kiliendeshwa na yule
broh wa chuo, alimhoji maswali magumu sana yule binti, binti kazungukaa weee
mwisho wa siku akanitaja mimi. Nilikataa kata kata maana nilikuwa najua
anaongopa. Majadiliano yalikuwa mengi na marefu, ila ukweli ukaja kugundulika,
aliyekuwa anaongoza mjadala (jamaa wa chuo) ndio muhusika wa ile mimba.
"Baada ya siku mbili, mzee jioni moja akaniita. Tukawa tumekaa nje,
tunaongea huku tunakunywa chai. Mzee alianzisha mada ambayo sikuitarajia.
Aliniambia "Katika maisha, ukiwa kama mwanaume hutakiwi kutembea na kila
mwanamke aliyekaribu na wewe, vinginevyo unaweza jikuta unapoteza watu muhimu
sana ambao wangeweza kuja kuwa msaada kwenye maisha yako".
"Tuliongea mengi, na alinipa hints nyingi sana. Ila wakati tunamalizia
maongezi, akaniambia nilifanya kosa kutembea na yule mfanyakazi wa ndani.
Nikashangaa why kasema vile. Alaf nikamkazia macho kwa msisitizo, huku
nikikataa zile tuhuma.
"Nilimwambia "Baba hadi
wewe unaamini nilitembea nae?". Mshua alitoa tabasam fulani hivi, ambalo
naweza sema ni la hudhuni, then akaniambia "MWANAMKE HAWEZI MSINGIZIA
MIMBA MWANAUME AMBAE HAJALALA NAE". Nilijisikia aibu sana, nikaondoka.
"Kiuhalisia, wanaume tumeumbwa na tamaa plus mioyo ya kutoridhika, hasa
linapokuja swala la mapenzi na wanawake. Utaoa leo, ila kesho mate yatakutoka
ukipishana na zigo jingine njiani.
"Ila from real life experience, naweza washauri sio kila mwanamke mzuri
anayekuwa in your life circle lazima upite nae. Why nawaambia hivi??
"Wote tunajua, ni nadra sana kukuta marafiki wakawaida wa jinsia tofauti
ambao hawana uhusiano wa kimapenzi wananuniana au kuchuniana. Ukitembea na
rafiki yako wakike, basi jua umegain mpenzi, ila umepoteza rafiki.
"Ukitembea na co-worker, basi jua umegain mpenzi na umepoteza co-worker.
Ukitembea na mfanyakazi wako, jua umepoteza mfanyakazi na umeongeza mpenzi.
Wote tunajua, palipo na mapenzi lazima vifuatavyo viwepo:
1. Wivu kupitiliza
2. Kununiana bila sababu
"Mapenzi yanapunguza sana ufanisi wa utendaji kazi, hasa endapo utataka
kufanya vyote kwa pamoja (Rejea mfano wa Ngoswe).
"Kuna ile dhana kwamba, ukiwa na ukaribu sana na demu alaf usimtongoze,
atakuona nyuki wa mashine. Hizi kauli zimelostisha wana wengi sana. Unamtongoza
demu anayekupaga deals, mkishakuwa wapenzi then mkagombana usitegemee akupe
tena zile deal.
"Hata uwe unatembea na pisi mpya kila wiki, hutoweza wamaliza wote, maana
on everage wapo wengi kutuzidi. Japo Opportunities are endless, ila ukianza
kutongoza kila unayemuona, slowly you will be blocking your connections.
"Nakumbuka kipindi nilipoamua kuondoka home baada ya kugoma kusoma HKL.
Mshua badala ya kunisihi nisikimbilie Dar na umri ule mdogo, tena bila ya kuwa
na ndugu, yeye alinikumbushia tena ili swala, then akaendelea na mishe zake
(nilisota sana huko nilipoenda, ila nikanyooka).
"Wakuu, kuwa mwanaume ni pamoja na kusimamia unachokipigania, kuweza
kucontrol hisia zako.
Regards.
Analyse.

Post a Comment