TETESI ZAMTAJA RONALDO KUSEPA JUVENTUS

WAKATI ligi nyingi kubwa barani Ulaya zikiwa zimemalizika na mabingwa wao kujulikana, kuna kila dalili kuwa mshambuliaji nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo ataondoka kukosini baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro.
Mkongwe huyo ambaye ameweka historia
ya kuwa mfungaji bora katika ligi tatu ngumu barani Ulaya, England, Hispania na
Italia, anatakiwa kubaki na kocha mpya Allegri, lakini Ronaldo ili abaki,
anataka Juve isajili wachezaji wapya wenye vipaji.
Ronaldo anaamini kutokana na umri wake anahitaji zaidi vijana
wenye vipaji vikubwa wakishirikiana nae ili waipeleke mbele Juventus.
Allegri amewaambia viongozi kuwa yupo tayari kufanya kazi na
Ronaldo au bila Ronaldo, anakiamini kikosi chake angependa Mreno huyo asalie
kikosini.
Tetesi kutoka watu wa karibu na CR7, PSG ni sehemu anayoweza
kwenda huku Manchester United ikiwa chaguo lake la pili.

Post a Comment