MPOKI ASEMA DIAMOND NI MSHINDI


Nyota wa Afrika mashariki na Mpoki - YouTube

MCHEKESHAJI mahiri nchini Tanzania, Mpoki amempongeza msanii Diamond Plutnumz kwa kuteuliwa kuwania Tuzo za BET mwaka huu akisema kitendo hicho pekee kimempa ushindi hata kama hatapata ushindi siku ya shughuli.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mpoki ameandika: ''09/Dec/1961 TZ ilipata Uhuru Mpk sasa inakadiriwa jumla ya Watanzania tunakaribia 60M, Lakini umekuwa Mtanzania mwingine kuchaguliwa ktk award kubwa zaidi Duniani (BET) hata usiposhinda kwetu sisi wewe ni mshindi thamani yako kubwa sana........tulipewa Akili,utashi na maarifa ili tuvitumie kwa Pamoja,,,,,,Hongera sana wengine ngozi zetu nyeusi ila Roho zetu nyeupe @diamondplatnumz @wcb_wasafi ''

No comments