INAKUAJE UNAMUUA MKEO/MUMEO?

MUME alirejea nyumbani kwa ajili ya chakula cha mchana akitokea kibaruani kwake. Kama ambavyo inakuwa siku zote, aliwapita akina mama majirani wakiwa wenye mashasha na, wakimuitikia kwa furaha salamu yake na wachache kati yao akitaniana nao.
Akaifikia nyumba
yake na kuingia sebuleni. Hakumkuta mkewe hapo sebuleni na kama ilivyo kawaida,
akaanza kuita, Baby...Baby...Baby... akielekea chumbani kwake.
Akamkuta mkewe
akiwa amejilaza kitandani, kama mtu mwenye uchovu mwingi. Akiamini
alijipumzisha kutokana na kazi nyingi za nyumbani, kwa kutumia simu yake,
akampiga picha, kisha akambusu na kumuomba akamuandalie chakula mezani.
Wakatoka wote
kuelekea sebuleni ambako baada ya mume kula na kushiba, akamshukuru mkewe na
kisha huyooo, akaelekea zake kazini ambako hakukuwa mbali na nyumbani. Masaa
mawili baadaye, akatoa simu yake na kuamua kumtazama mkewe katika picha
aliyompiga.
Alitaka auone uzuri
wake akiwa hajajipamba. Alitaka auone ubaya wa mkewe akiwa hajavaa sura ya
vipodozi, alitaka aione sura yake ikiwa orijino. Ghafla akashtuka, mapigo ya
moyo wake yakaanza kupiga kwa nguvu. Akaizoom picha. No....hakutaka kuamini.
Akaizima simu na
kuiwasha tena. Akairudisha picha ya mkewe, akaitazama tena. Yes, alichokiona
mwanzo ndicho alichokiona sasa. Hasira zikampanda, akaanza kutetemeka.
Kwenye kabati
ofisini kwake, akaifungua na kutoa bastola yake. Akaifutika kiunoni, akatoka
nje na kuipungia bodaboda, ikaja na kumpeleka nyumbani. Aliingia ndani kwake
akiwa amevurugwa. Akamkuta mkewe sebuleni, tabasamu tele usoni.
Akapitiliza
chumbani kwake, akalifunua godoro, hakuona kitu. Akarejea sebuleni kwake,
akatoa bastola yake na mkewe akiwa ameduwaa, alishuhudia risasi ikipasua kichwa
chake. Akafa palepale...
Kwa nini alimuua?
Katika ile picha aliyompiga aliporudi kwa chakula, baada ya kuitazama vizuri,
aliona kuna mwanaume alikuwa amejificha uvunguni mwa kitanda, akionekana sura
kwa mbali. Alipoitazama vizuri, alimtambua mwanaume huyo, ni mtu anayemfahamu
na kumheshimu!
Mlio wa risasi
mbili pale sebuleni, iliwashtua majirani. Kwa tahadhari, wakafika nje na kuanza
kubisha hodi. Mume alijitokeza akiwa amenyoosha mikono yake juu, tayari
kuikabili hukumu yoyote iliyo mbele yake. Kuona hivyo, majirani wakaingia ndani
na kushuhudia mwili wa mke ukiwa umelala sebuleni, damu nyingi zikivuja kutoka
kichwani.
Wakajiuliza, nini
kimetokea? Mbona dakika saa chache zilizopita, watu hawa wawili walikuwa na
furaha tele?
Kipo kitu cha
kujifunza. Mambo ya ndani ya nyumba, ni siri kubwa ambayo wakati mwingine hata
watoto wa kuwazaa wasijue. Watoto wanaweza kuona wazazi wanagombana, lakini
wasijue chanzo.
Yule mwanaume
aliyekuwa ndani na marehemu, ni kaka wa mumewe, aliyekuwa akiishi jirani nao.
Walikuwa na tabia za kutembeleana mara kwa mara na majirani wote walifahamu
hivyo. Ni vipi walianzisha uhusiano wa kimapenzi na shemeji yake, si jambo
muhimu kwa sasa. Lakini ujumbe ni kwamba usije ukasema haiwezekani kwa jambo
lolote.
Tabia kama hizi, za
mume kutembea na mdogo au dada wa mkewe au mke kutembea na mdogo au kaka wa
mumewe, ni za kawaida katika jamii zetu. Achilia mbali kutembea na mume au mke
wa rafiki yake, jirani yake au hata mfanyakazi mwenzake.
Na katika hali ya
kushangaza zaidi, wapo watu wanatembea na wakwe zao, yaani mume au mke wa
mwanaye. Kuna ushetani wa kutisha, kwani baadhi hutembea na hata watoto wao wa
kuwazaa!
Na bahati mbaya
sana, kwenye mahusiano haya, majirani huwa wanajua. Ni rahisi kumkuta mtu
anakuambia, 'unamuona huyo mama, anatembea na shemeji yake' au 'huyo jamaa hapo
bwana noma sana, anamla mdogo wa mkewe'.
Wanajuaje mahusiano
haya, pia siyo jambo la msingi kwa sasa. Ujumbe wangu ni kwamba kuna mambo
mengi sana machafu, yasiyo ya kimaadili tunayafanya huku mitaani, ambayo
tukisikia tunayaona ya ajabu, wakati yanafanyika kila siku.
Kinachofanya wakati
mwingine mume au mke kumuua mwenzake, wala siyo sababu za wivu wa kimapenzi
kama tunavyopenda kurahisisha, bali ni kwa nini atembee na huyu? Mtu ambaye
alikuwa akimchukulia kama spesho sana.
Chukulia kwa mfano
wewe mume, mkeo anatembea na mdogo wako uliyemleta mjini ili aendelee na
masomo. Kwa vyovyote, dogo hawezi kumtongoza shemeji yake, isipokuwa shemeji
mtu alitengeneza mazingira ya kumshawishi bwana mdogo.
Au wewe mke, mumeo
anatembea na mama yako mzazi. Kwa namna yoyote, alikuwa na kila sababu ya
kukataa uhusiano huo kama alishawishiwa, lakini kwa kukubali, maana yake ni
kuwa ameidhalilisha familia yao.
Ni kweli, katika
uhusiano wa kimapenzi, zipo sababu nyingi zinazoweza kuwafanya watu
wakorofishane, lakini nyingi kati ya hizo, husababishwa na uhusiano wa
kimapenzi na watu wengine, hasa walio karibu yao!

Post a Comment