DIAMOND AIPONGEZA SIMBA, SENZO ATAKA CHAMA, KAPOMBE WAENDE TIMU KUBWA ZAIDI


Kapombe Soka lake limempa mijengo ya maana - Mwanaspoti

KUFUATIA kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa timu ya Simba na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, msanii Diamond Platnum amewapongeza wekundu hao wa Msimbazi, akisema pamoja na kupoteza lakini walipambana kibingwa kwa ushindi wao wa mabao 3-0.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliandika:
"Kwa kazi mliyoifanya leo... Penati ya wazi tuliyonyimwa, na magoli lukuki tuliyowakosa 
@kcfcofficial...Ni dhahiri kabisa kuwa ni mwenyezi mungu alipanga @kcfcofficial waende wao nusu fainali....Lakini wanangu mmepambana, mmefanya kazi kubwa na mmedhihirisha kuwa simba ni team bora!!"

Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo ya Simba, Senzo Masingisa ambaye hivi sasa yupo Yanga, ametoa maoni yake akiwashukuru wachezaji aliowahi kufanya nao kazi kwa namna wanavyojituma na kusema wapo ambao wanastahili kuchezea timu kubwa zaidi ya Simba.

Amewataja baadhi yao kuwa ni pamoja na Aishi Manula, Clatus Chota Chama, Paschal Wawa, Shomari Kapombe na Louis Miquissone.

Katika mchezo huo wa marudiano, Simba ilipata ushindi wa mabao 3-0 baada ya hapo awali, kubugizwa mabao 4-0 kule bondeni.

No comments