WAKIMBIAJI 21 WAFA GHAFLA CHINA

KUFUATIA hali ya hewa kubadilika
ghafla, kutoka joto la kawaida hadi mvua ya mawe yenye baridi kali, wanariadha
21 wamepoteza maisha wakiwa mashindanoni (Ultramarathon) katika jimbo la Gansu,
nchini China.
Maafisa wa eneo hilo wanasema mbio hizo zilizojumuisha Watu
172 ziliathiriwa ghafla na hali mbaya ya hewa ambapo ndani ya kipindi kifupi
Joto lilipungua na kutokea mvua ya barafu.
Washiriki kadhaa walituma ujumbe wakiomba msaada na kufuatia
hali kuendelea kuwa mbaya waandaaji waliahirisha mbio hizo na kutuma timu za
waokoaji.

Post a Comment