CRISTIANO RONALDO: MWANASOKA TAJIRI MWENYE MOYO WA KUTOA AKIGUSWA

KUNA wanasoka wengi waliopata pesa kutokana na uwezo wao uwanjani, wakilipwa mamilioni kila siku, wiki, mwezi na kwa mwaka. Miongoni mwa hao, ni Mreno, Cristiano Ronaldo ambaye ni tajiri miongoni mwa wachezaji wakubwa duniani.
Amefanya mengi kuthibitisha namna
anavyoguswa na matatizo ya watu wengine, hasa wale ambao hawana uwezo kama
wake.
Miaka kadhaa nyuma uwanjani Estadio Di Dragao Jijini Lisbon
Ureno, wakati timu ya taifa ya Ureno ikifanya mazoezi, ghafla aliingia mchezaji
Carlos Martins ambaye alionekana mnyonge sana, Ronaldo alikuwa wa kwanza
kumfuata.
Alimuuliza Martins shida nini? Martins alieleza kuwa mwanae
anaumwa sana, ana upungufu wa bone marrows (uroto) anapaswa kuchangiwa, Ronaldo
bila kusita akahimiza na wachezaji wengine wakaelekea hospital kumchangia kijana.
Mwaka 2007, Cristiano Ronaldo alilazimika kusafiri mpaka
Asia, baada ya mwandishi mmoja kumpiga picha mtoto alietelekezwa wakati wa
Tsunami kali, mtoto alikuwa na jezi ya Ronaldo mgongoni, hiyo ilimgusa sana na
anamsomesha mpaka leo, yupo Ureno
Miaka kadhaa mbele, aliwahi kuhojiwa Cristiano Ronaldo
kwanini hana mchoro wowote mwilini (tattoo) aliweka wazi kuwa adhma yake ni
kuwa Mchangiaji wa damu kwa maisha yake yote, angechora tattoo maana yake
angekosa sifa ya kuchangia.
Mwaka 2011 baada ya kubeba kiatu cha dhahabu cha wafungaji
Bara la Ulaya, wakati anarudi nyumbani alisikia taarifa redioni juu ya uhaba wa
huduma za Kijamii kule Ukanda wa Gaza, changamoto ya shule, hospital na maji.
Ronaldo alimuagiza wakala wake, Jorge Mendez achukue kiatu
chake cha dhahabu kikapigwe mnada kisha pesa ile yote ipelekwe Gaza, ilipatikana
kweli Pauni 1.5 Million na Mendez akaipeleka Gaza ili iwasaidie watoto kule
kupata huduma zote za kijamii kwa wakati sahihi
Wakati shirika la SAVE THE CHILDREN linapambana kusaidia
watoto nchini Nepal 2015, Ronaldo aliguswa mno na harakati zile, ikalazimika
asaini cheki ya Pauni Million 5, pesa hiyo ilisaidia kwa asilimia kubwa kwa
watoto kule nchini Nepal.
Juzi kile kitambaa alichotupa kwa hasira pale Serbia
kiliokotwa na Mfanyakazi wa uwanja huo na kukipeleka kwenye Asasi za Kijamii na
kikapigwa mnada kusaidia upasuaji wa watoto kule Belgrade, na inasemekana
kiliuzwa kwa bei ya juu sana.
Credit: Shaffi Dauda

Post a Comment