WAVUNJA ZEGE KUBOMOA KABURI LA ALBINO, WATOKOMEA NA VIUNGO VYAKE


Watu wasiojulikana wamevunja zege lililowekwa kwenye kaburi la mtu aliyekuwa na ulemavu wa ngozi na kuondoka na baadhi ya viungo vyake, tukio lililotokea huko Magharibi mwa Msumbiji.

Viungo vya miili ya albino vinatafutwa sana nchini humo kwa ajili ya matumizi ya imani za kishirikina.

Polisi wanasema washukiwa bado wanazuiliwa baada ya tukio hilo wilayani Moatize, mkoani Tete.

Marehemu ambaye alikuwa na umri wa takriban miaka 50, alizikwa hivi karibuni katika kijiji kinachopakana na Malawi.

Ndugu zake walikuwa wamelijenga kaburi kwa zege ili kuzuia uwezekano wa wizi ambao ungeweza kutokea.

Mwanaharakati wa haki za albino, Remane Madane, amelaani wizi huo.

Alisema polisi waliahidi kufanya kila linalowezekana ili kuwakamata washukiwa hao.

"Makaburi yametengwa. Kufika huko ni umbali mrefu, kwenda peke yako lazima ufikirie mara mbili, vinginevyo labda timu ilihusika,” alisema.

Watu wenye ualbino, wanauawa mara kwa mara katika nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Malawi, Msumbiji na Tanzania.

 

No comments