Watumishi wa CCM Pwani wafundwa


Watumishi wa CCM Mkoa wa Pwani wametakiwa kutojihusisha na ushabiki wa kuweka mawazo yao kwa watu badala ya CCM wakati wa chaguzi zijazo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani *ndugu* *Mwinshehe Mlao* wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku ya Moja ya watumishi hao yaliyofanyika tarehe *18/12/2023* Wilayani Mkuranga Mkoani humo.

 *Mlao* amesema wako baadhi ya watumishi wameanza kuweka mawazo yao kwa watu kwa ajili ya uchaguzi ujao  jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa Kanuni, miongozo na taratibu za Chama.

Amesema watumishi wanatakiwa kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kuleta athari kwa Chama na utumishi wao huku akiwataka mawazo yao kuyaelekeza kwenye Chama zaidi kuliko watu binafsi.

Ameendelea kusema kuwa Kila mtumishi ana wajibu wake unaomzid mwingine katika kutekeleza majukumu ya hivyo kuwahimiza kusimama katika nafasi zao ili kukijenga Chama.




Pia amesema Kila mtumishi ana thamani kwa mwenzake hivyo aliwaasa kutodharauliana na badala yake kuheshimiana na kusaidiana.

 *Mlao* amesema wanaccm wanaohitaji kukisaidia Chama wasizuiliwe badala yake wafuate taratibu za vikao katika ngazi husika na kuongeza kuwa Chama hakiwezi kujengwa na mtu mmoja.

Aidha amewasisitiza watumishi hao kuendelea kutunza siri za vikao hasa unapofika wakati wa chaguzi mbalimbali.

Amehitimisha kwa kuwapongeza watumishi kwa kufanya kazi kwa bidii huku akiwakumbusha Kila mmoja kwa nafasi yake ajipange na chaguzi zijazo kutengeneza mikakati ya kukipatia Chama ushindi.


Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  *Bi *Khadija* *Nassir* amewaeleza watumishi wa CCM Mkoa wa Pwani kujitambua kuwa wao ni kioo katika utumishi wao na wanategemewa katika kuhakikisha Chama kinafikia malengo yake.

Akizungumza na Watumishi hao wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya siku Moja *Bi *Khadija* amesema CCM imewapatia heshima kubwa ya kuteuliwa hivyo wanatakiwa kusimamia maslahi ya Chama kikamilifu na si vinginevyo.




 *Bi Khadija* amesema kila mtumishi anatakiwa kutekeleza majukumu yake na kuiheshimisha CCM huku akiwaambia kuendelea kuwa na utaratibu wa kusikiliza na kuheshimiana.

Pia amesema Kila Mtumishi ana haki ya kuitwa mtu fulani kinachotakiwa ni kurudi kwenye mstari na kuyasimamia majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Ameendelea kusema kuwa uongozi ni duara na kuwasihi kutoinua mabega kwa vyeo vyao na kujitahidi kutunza siri za viongozi kwani usiri ndio mafanikio ya taasisi au mtu binafsi.

Amemalizia kwa Kumpongeza *Mhe* *Daktari Samia Suluhu* *Hassan* Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha kazi za maendeleo kwa asilimia mia Moja.


 *Taarifa hii imeandaliwa* *na:* 


David Mramba

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM

Mkoa wa Pwani.

No comments