UJUMBE WA LEO
Waswahili wanafiki huwa wana
misemo yao miwili mikuu.
1. Tupo nyuma yako
2. Tupo pamoja
Kiasili waswahili ni wanafiki sana. Na miaka ya hivi karibuni wamekosekana kabisa
watu wenye uthubutu, kujiamini, misimamo na ujasiri.
Wamebaki watu ambao watakwambia "endelea mbele tupo nyuma yako"
usishangae ukageuka ukajikuta upo peke yako wakati ambao sasa uliwahitaji kweli
kweli.
Miaka hii kwa sababu ya unafiki wamekosekana watu wa kuwa nawe bega kwa bega.
Hawa wanaokuwa nyuma yako huwa wanapima tu upepo unavyoenda. Wewe ndo
wanakutanguliza kama chambo.
Lakini pia kumbuka kuna wale wanakuwa nyuma yako ili waokote unavyodondosha.
Hawa ni mafisi, hawa ni wenye uchu. Hawataki muwe sambamba. Wanataka
unachodondosha ndo waokote watakusisitizia nenda baba nenda upo sahihi sisi
tupo nyuma yako. Achana na marafiki, wafuasi wanaokaa nyuma yako.
Tafuta watu ambao mtakuwa nao sambamba, bega kwa bega ili wakisita uone kuwa
umewaacha nyuma. Au wakipandisha morali utaona wanaanza hata kukuacha wewe.
Hawa watakutia moyo unapokuwa umechoka.
Walio nyuma yako hawa hupunguza mwendo nawe. Ukisimama nao husimama na ukigeuka
watakwambia usijali. Tupo nyuma yako. Ukiangalia huoni wanachofanya cha maana
nyuma yako.
"Mwenye Meno akicheka, Mwenye
Mapengo Huudhika "

Post a Comment