SIMBA YAENDA KUKAMILISHA RATIBA CAIRO

 


Simba SC vs Al Merrikh: TV channel, live stream, team news and preview |  Goal.com

 

KWA mara ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania, klabu yake inaingia katika hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika ikiwa inaongoza kundi lake.

Simba ndiyo imekuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kufanya hivyo, tena ikiwa na mechi moja mkononi. Wakiwa safarini kuelekea Cairo nchini Misri, mabingwa hao mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 13 baada ya mechi tano.

Wanakwenda Cairo nchini Misri kupambana na mabingwa watetezi wa klabu bingwa Afrika, Al Ahyl, katika mechi ambayo matokeo yake yoyote hayawezi kuathiri uongozi wa Simba, kwani hata wakifungwa, watakuwa mbele kwa alama mbili.

Mechi hiyo ya kukamilisha ratiba itafanyika Jumamosi hii na wengi wanataraji wekundu hao wa Msimbazi kuweza kuweka rekodi nyingine baada ya kuwa klabu ya kwanza Tanzania kuongoza hatua za makundi ikiwa na mechi moja mkononi, kucheza mechi tano za mashindano hayo ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja, kufungwa mabao machache zaidi kuliko timu zote na kucheza kwa kiwango kikubwa (ball possession) katika mechi zote.

 

No comments