RIPOTI YA CAG INACHANGANYA
RIPOTI ya Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayoonyesha ufisadi wa kiwango
cha juu cha fedha za serikali, umewachanganya wananchi, wasiamini kama jambo
hilo limeweza kufanyika enzi za utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe
Magufuli.
Katika ripoti hiyo,
imeonyesha ufisadi katika baadhi ya maeneo ambayo inaaminika yalikuwa chini ya
uangalizi makini wa JPM mwenyewe, kama ATCL ambako shilingi zaidi ya bilioni
tatu 'zilipigwa' kwa ajili ya matengenezo ya ndege, ambayo kumbe imepaki tangu
mwaka 2015.
Hiyo ni mbali na
hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 153 ndani ya miaka mitano ya utawala wa
kiongozi huyo aliyekuwa na sifa ya ukali.
Aidha, serikali
imepata hasara ya mabilioni katika mradi wa Bwawa la Umeme la Mto Rufiji, baada
ya kubainika wageni zaidi ya 1500 wanafanya kazi bila kuwa na vibali vya
kuwaruhusu kufanya kazi nchini.
Eneo jingine
lililowachanganya wananchi, ni ripoti kuwa fedha zilizopigwa na wajanja,
zilipitia katika akaunti ya Jeshi la Uokoaji, jambo ambalo haieleweki ni katika
mazingira gani jambo hilo liliwezekana.

Post a Comment