SERIKALI KUWASILISHA MUSWADA WA KUREKEBISHA KIKOKOTOO CHA MAFAO

Serikali imeliambia bunge kuwa lipo katika hatua za mwisho
kwa ajili ya kuwasilisha bungeni muswaada wa marekebisho ya sheria ya mafao ya
wafanyakazi kuhusu kikokotoo kipya baada ya kukamilisha vikao vinavyowahusisha
viongozi wa vyama vya wafanyakazi na kuwa na sheria isiyoweka vikwazo kwa
wafanyakazi kuchukua fedha zao pindi wanapostaafu.
Waziri wa Nchi Sera, Uratibu bunge vijana ajira na watu wenye
ulemavu Mhe Jenister Muhagama ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya
matumizi ya bunge baada ya mbunge wa viti Maalumu Chadema Mhe Ester Bulaya
aliyetaka kujua lini serikali itaondoa kizungumkuti cha kikokotoo kipya
kilichosimamishwa na mwaka 2018 na Hayati Rais Dokta Jonh Magufuli baada ya
kulalamilikiwa na wastaafu kukatwa fedha zao kwa kutumia kikokooti kipya.
Katika hatua nyingine serikali imeweka kisera suala la lishe
bora kwa wananchi katika mpango wa taifa wa miaka mitano kutokana na tatizo la
udumavu kwa watoto kwa kukosa lishe na kuendelea kukabili zaidi mikoa
inayozalisha chakula kwa wingi ikiwemo Iringa, Songwe na Ruvuma.
ITV

Post a Comment