HATUUZI WACHEZAJI
CEO wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez, amesema kwa sasa hawana mpango wa kuuza wachezaji hadi pale watakapokuwa wamehakikisha wametwaa ubingwa wa Afrika, ndipo wataanza biashara hiyo.
Barbara ametoa kauli hiyo wakati Simba ikiwa tayari imeingia hatua ya robo fainali na ikiwa na mechi moja mkononi ya leo usiku dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahyl ya Misri, pambano ambalo litachezwa katika uwanja wa klabu hiyo jijini Cairo.
Kwa mujibu wa utaratibu wa michuano hiyo ya Klabu Bingwa Barani Afrika, mojawapo ya motisha ya timu inayoongoza kundi, kama ilivyo kwa Simba mwaka huu, ni kuanzia mchezo wake wa kwanza ugenini na kumalizia nyumbani.

Post a Comment