WAZIRI CHAMURIHO ATAKA TAASISI ZA UJENZI, UCHUKUZI KUWAJIBIKA
Wakurugeni
wa Wizara, Wakuu wa Vitengo pamoja na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara
wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuz iMheshimiwa Dkt. Leonard Chamuriho
(hayupo pichani), katika kikao kazi kilichowakutanisha
viongozi hao jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,
Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amewataka Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara
yake kuhakikisha wanaandaa taarifa kila mwezi zinazoelezea utekelezaji wa majukumu
yao ili kusaidia Wizara kufahamu kwa undani utendaji wa Taasisi hizo ikiwemo mafanikio
na changamoto zake.
Hayo aliyasema Waziri
huyo, jijini Dodoma, katika kikao kazi cha kumtambulisha NaibuWaziri wa Wizara
hiyo Mhe. Mwita Waitara, kwa mara ya kwanza kwa viongozi wa Taasisi hizo ambapo
pamojana mambo mengine amesisitiza kuwa Wizara itakuwa inaandaa vikao kama hivyo
mara nne kwa mwaka ili kujadiliana kwa pamoja na kupata tathmini na
mwelekeo wa Wizara katika ufanisi wake wa utendaji kazi.
"Nimeamua leo kuitisha kikao hiki ili kumtambulisha
Naibu Waziri kwa wakuu wa Taasisi zilizo
chini ya Wizara yangu, pia kukumbushana kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali
yaliyo katika Taasisi zao", amesema Waziri Chamuriho.
Aidha, Chamuriho amezisisitiza Taasisi hizo
kushirikiana na kuwajibika ipasavyo katika miradi wanayoitekeleza kwani mingi huigusa
jamii ambapo ameongeza kuwa, kufanya hivyo
kutapelekea maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake,
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mwita Waitara, amewataka viongozi hao wa Taasisi
kumpa ushirikiano wa kutosha na kwamba ofisi yake itakuwa wazi kwa ajili ya kupokea
ushauri na maoni mbalimbali lengo likiwa ni kusaidia kufanikisha utekelezaji
wa miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara hiyo ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Naomba Wakuu wa Taasisi
wanipe tu ushirikiano wa kutosha na niwabainishie kuwa Ofisi yangu itakuwa wazi
wakati wote kwa ajili ya kupokea ushauri lengo likiwa ni kuleta tija na maendeleo
kwa wananchi”, amefafanua NaibuWaziri Waitara.
Naye, Msajili wa Bodi
ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Arch. Edwin Nunduma,
amesema kuwa agizo hilo la Waziri la kuleta taarifa za utekelezaji Wizarani litawafanya
kuwajibika zaidi kutokana na kuwa Wizara itafuatilia kwa karibu utendaji wao.
"Utaratibu huu ni
mzuri, kwani hata changamoto zikitokea itakuwa
ni rahisi kuzitafutia ufumbuzi mapema na
kwa haraka", amesema Nunduma.
Kikao hiki cha siku moja
ambacho kimemkutanisha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mheshimiwa Dkt. Leonard Chamuriho, NaibuWaziri wa Wizarahiyo,
Mhe.Mwita Waitara, Menejimenti ya Wizara hiyo pamoja na viongozi wakuu wa Taasisi
23 zilizo chini ya Wizara hiyo, kilikuwa na lengo la kutambuana na kukumbushana
kuhusu uwajibikaji katika Taasisi zao.
Imetolewana Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Post a Comment