Shahidi: Sean "Diddy" Combs alinining'iniza kwenye ghorofa

 


Mbunifu wa picha Bryana Bongolan ametoa ushahidi mahakamani kwamba Sean "Diddy" Combs aliwahi kumning'iniza kwenye roshani ya ghorofa ya 17, na kwamba alimwona akimrushia kisu rafiki yake Casandra Ventura.

Siku ya Jumatano, waendesha mashtaka walionyesha picha zilizopigwa na Bi Bongolan na Diddy ambaye alikuwa mpenzi wake wa wakati huo za michubuko ya Bi Bongolan, ambayo alidai kuwa aliipata wakati wa tukio hilo linachodaiwa kutokea mwaka 2016.

Mawakili wa Combs walielezea kuwa na mashaka ya uaminifu wa Bi. Bongolan.

Combs anakabiliwa na mashtaka ya ulaghai, kula njama na biashara ya ngono. Amekana kuhusika na hatia yoyote.

Kesi hiyo ya serikali, ambayo sasa iko katika wiki ya nne ya ushuhuda, ilifuatia kesi kadhaa za madai zilizowasilishwa dhidi yake na wanaume na wanawake wakimtuhumu kwa unyanyasaji, akiwemo Bi Ventura, ambaye ni mpenzi wa zamani wa Combs, na Bi Bongolan.

No comments