DR Congo yapiga marufuku kuripoti habari za rais wa zamani Josep Kabila

 


Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo(DRC) imevipiga marufuku vyombo vya habari kuripoti shughuli za Rais wa zamani Joseph Kabila na kuwahoji wanachama wa chama chake.

Haya yanajiri baada ya Kabila kurejea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi uliopita huku akiwa na mvutano mkali kati yake na serikali, inayoongozwa na mrithi wake, Rais Félix Tshisekedi.

Mamlaka zinashinikiza kumfungulia mashtaka Bw Kabila huku kukiwa na tuhuma za uhaini na madai ya kuwa na uhusiano na waasi wa M23 ambao wamekuwa wakipigana na jeshi - jambo ambalo amelikanusha hapo awali.

Ukiukaji wa marufuku hiyo unaweza kusababisha kusimamishwa, alisema mkuu wa udhibiti wa vyombo vya habari nchini DRC, Christian Bosembe.

Ikijibu tangazo la taasisi hiyo, msemaji wa M23 alisema vyombo vya habari katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake havitatii marufuku hiyo.

No comments