Vigogo wajiondoa Chadema
Akitangaza uamuzi huo, Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara alikuwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita.
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?
G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.
Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)

Post a Comment