Wajasiriamali Pwani wataka serikali kuiwekea mazingira wezeshi


ILI kuhakikisha wajasiriamali Mkoani Pwani wanakuwa serikali itaendelea kushirikiana nao kwa kuwawekea mazingira wezeshi.

Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashid Mchatta alipokuwa akikabidhi vyeti kwa wajasiriamali waliotambuliwa na Shirika la Viwanda Vidodovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani. Mchatta amesema kuwa pia watahakikisha wanazingatia mbali ya ubora na viwango ili waweze kuziuza ndani na nje ya nchi na kushindana kwenye masoko makubwa na kukuza uchumi wa watu mkoa na nchi.


Amesema kuwa SIDO imefanya kazi kubwa kuwapatia mafunzo na mitaji kwa ajili ya wajasiriamali ambao wameanzisha viwanda vidogo na kuisaidia serikali kuongeza ajira. Aidha ameipongeza SIDO kwa jitihada za kuwawezesha wajasiriamali ambapo Mkoa huo una jumla ya viwanda 1,533 vikubwa 122 vya kati 120 vidogo 274 na vidogo sana 1,117. Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Pwani Beata Minga amesema kuwa unatambua jitihada za wajasiriamali ambao wameanzisha viwanda ambavyo vitaongeza ajira na kuongeza pato la mwananchi mkoa na Taifa. Minga amesema kuwa vyeti hivyo vya kuwatambua vitawasaidia pale wanapohitaji kutambuliwa na taasisi nyingine ambazo ni za uwezeshaji na zoezi hilo litakuwa endelevu ambapo jumla ya wajasiriamali 65 wametambuliwa.

No comments