Step by Step yamalizia Tarafa ya Ruvu Kibaha Vijijini leo
Ziara ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Pwani, David Mramba leo itamaliza katika Tarafa ya Ruvu iliyopo Kibaha Vijijini kwenye Kata nne.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Katibu wa Itikadi mkoani Pwani, leo ziara hiyo itafanywa katika kata za Magindu, Boko, Gwata na Soga.
"Ziara hii imekuwa ya mafanikio makubwa kwani licha ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, watu wamejitokeza kwa wingi na kupata mafunzo ya itikadi na namna ya kukijenga chama katika mkoa huo," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Ziara hiyo ambayo imebeba kauli mbiu ya Step by Step, pia inalenga kuifanya Pwani kuwa ya kijani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Post a Comment