Serikali kujenga maabara ya kisasa ya upimaji wa sampuli za madini nchini
-_Waziri Mavunde aitaka GST kuwa sehemu ya kwanza ya taarifa sahihi za maabara_
-_Maabara kuwekwa vifaa na mitambo ya kisasa_
-_Watumishi GST kujengewa uwezo zaidi_
-_Maabara za Kanda kujengwa ili kusogeza huduma karibu kwa wachimbaji_
Waziri wa Madini *Mhe.Anthony Mavunde* amesema kuwa serikali chini ya uongozi wa *Mh Rais Dkt. Samia Suluh Hassan* imejipanga katika mwaka wa fedha 2024/25 kuanza ujenzi wa maabara kubwa na ya kisasa na yenye vifaa vya kisasa itakayojengwa katika eneo la Kizota jijini Dodoma ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Sekta ya Madini nchini na matarajio ya wadau kwa ujumla.
Ujenzi huu wa maabara kubwa na ya kisasa utaenda sambamba na ujenzi wa maabara za kanda na kuwajengea uwezo watumishi wa GST ili kuendana na kasi kubwa ya maendeleo ya Teknolojia duniani.
Mh. Mavunde ameyasema hayo jana Aprili 24, 2024 jijini Dodoma katika kikao cha pamoja cha kujadili namna bora ya utendaji kazi kilichowakutanisha

Post a Comment