Makonda: Kuna Mawaziri wanawalipa watu wamtukane Rais Samia mitandaoni
Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya jumatatu tarehe 14 April 2024.
Hizi ni moja kati ya tuhuma nzito zaidi kuwahi kutolewa na Makonda kwa viongozi waandamizi wa serikali ya awamu ya sita, tangu alipoteuliwa kurejea tena katika uongozi baada ya kuwa ameachwa nje ya Rais John Pombe Magufuli.
Akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, mara kadhaa akiwa katika ziara mikoani, Makonda aliwahi kuatuhumu watendaji wa serikali kushirikiana na walio nje ya mfumo katika kuminya haki za wananchi, ikiwa ni pamoja na kusababisha migogoro ya ardhi, utoaji wa haki na rushwa.

Post a Comment