CCM YACHANGIA TSH MILIONI 10 KWA WANANCHI WALIOPATWA NA MAAFA YA MAPOROMOKO YA MLIMA - ITEZI MKOANI MBEYA

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi , amewatembelea wananchi waliopatwa na maafa ya kuharibikiwa kwa nyumba na mali zao mara baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini na kusababisha maporomoko ya matope kutoka kwenye Mlima Kawetere, Kata ya Itezi, jijini Mbeya.

Mara baada ya kufika kwenye kambi wanaoishi kwa muda katika Shule ya Msingi ya Tambukareli , Baloz Nchimbi ametanguliza salamu za pole za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan , na kuwapatia kiasi cha Tsh Milioni 10 waathirika  hao ili kupunguza madhila yanayowakabili.

Balozi Nchimbi alikabidhi fedha hizo  kusudi  kwa mwanamama mmoja kati ya waliopatwa na maafa hayo pamoja na Diwani wa kata hiyo ya Itezi, Sambweshi Tambala ambaye pia amepatwa na maafa.

Akizungumza na wananchi hao, Balozi Nchimbi amesema lengo la kufika hapo ni kuwapa pole na kuwaomba kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

No comments