Yanga, Asec Mimosas watamaniana
Kwa mujibu wa Utaratibu wa CAF, timu nne zilizoongoza makundi zinacheza na timu nne zilizoshika nafasi za pili katika makundi yao, kwa maana timu zilizoongoza haziwezi kukutana zenyewe kwa zenyewe kama ilivyo kwa timu zilizoshika nafasi za pili.
Asec ni moja kati ya timu nne zilizoshika nafasi ya kwanza kwenye hatua ya makundi, zingine zikiwa ni Al Ahyl ya Misri, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Petro de Luanda ya Angola. Yanga kwa upande wake, ni miongoni mwa timu zilizoshika nafasi ya pili, zingine zikiwa ni Simba ya Tanzania, TP Mazembe ya DR Congo na Esperence de Tunis ya Tunisia.
Yanga hawawezi kukutana na Al Ahyl kwa sababu walikuwa kundi moja, hivyo wao watakutana na moja kati ya vinara wa makundi ambao ni Mamelodi, Petro de Luanda au Asec. Kwa kutambua kuwa timu hizo mbili za kusini mwa Afrika ni maji marefu, Wananchi wanaombea wakutane na wababe wa Ivory Coast, kwani wanaonekana kama wanaweza kuwamudu.
Na kwa upande wa Asec, hawataweza kukutana na Simba kwa vile walikuwa kundi moja, hivyo washindani wao ni Yanga, TP Mazembe au Esperance. Sasa Asec wanaomba wapangiwe Yanga, kwani kwao, hao ndiyo timu dhaifu kuliko zilizobaki.

Post a Comment