DC Mbinga akabidhi vitabu, taulo za kike kwa shule 164 vyenye thamani ya milioni 22
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Ally Mangosongo amekabidhi vitabu vya kiada na taulo za kike kwa wakuu wa shule za msingi 165 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga vyenye thamani ya shilingi milioni 22, huku akisisitiza vifaa hivyo vikatumike kwa malengo husika sambamba na vitabu hivyo kitunzwa vizuri.
Akikabidhi vifaa hivyo Mhe.Mangosongo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mhe.Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kuboresha miundombinu ya vyoo, madarasa na madawati na sasa vitabu lengo kubwa ni kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi ya kujifunzia na kufundishia kwa walimu na wanafunzi ili kuongeza ufaulu.
Hivyo basi, Aliwataka walimu vitabu hivyo vikawe nyenzo muhimu ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa darasa la 1,2 na 3 ili kuondoa utoro na kuchochea kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao kwa kuzimudu vizuri stadi za kusoma, kuandika na kusoma.
Aidha, Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kaimu Mkurugenzi Andrew Mbunda kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Ndugu Juma Haji, Alibainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya Mbinga imepokea vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya shule za msingi 164 kati ya 165 Isipokuwa shule ya msingi kilango ambayo imesajiliwa karibuni, vyenye thamani ya tzs milioni 22 kwa ajili ya darasa la awali, 1, 2, na 3 pamoja na taulo za kike kwa watoto ambao wameanza balehe.
Mwisho, Naye Agnes Mpika Kwa niaba ya walimu wengine walimshukuru Mhe.Rais,Dkt Samia Suluhu Hassan, Kwa kutoa fedha kwa ajili ya miundombinu ya madarasa na vyoo na sasa vitabu ambavyo vitaongeza ufanisi kwa wanafunzi kujifunzia ili kuongeza ufaulu na kukuza bora wa elimu inayotolewa shuleni.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbinga.
March 05, 2024.

Post a Comment