WATENDAJI WA CCM MKOA WA PWANI WAPATA MAFUNZO YA JINSI YA KUANDAA VITABU VYA FEDHA

 


Watendaji wa CCM Mkoa wa Pwani tarehe 21/03/2024 wamepata Mafunzo ya namna ya kuandaa vitabu vya fedha katika miradi iliyopo katika maeneo yao.


Akitoa Mafunzo hayo ndg Stephano Mayani kutoka Makao Makuu ya CCM Dodoma amesema iko sababu ya Kila mtendaji kuendelea kujifunza namna ya kuwa na kumbukumbu ya vitabu vya fedha kutokana na miradi au kupokea fedha kutoka kwa wahisani na wadau mbalimbali.


 Ndg. Mayani amemalizia kwa kusema watendaji wanapaswa kuwa na kiu ya kujifunza mara kwa mara ili kuwa na uelewa zaidi kuhusu kumbukumbu za kifedha.







Taarifa hii imeandaliwa na:

David Mramba
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM
Mkoa wa Pwani.



No comments