Wakamatwa kwa kujitangaza kutoa huduma ya internet ya Starlink Instagram
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum SACP Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.
Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebanika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Jamii Forum

Post a Comment