Jukwaa Wazalendo huru Tanzania lapanda miti 300 Mtongani Kibaha Pwani



Na Madam Mariam Msede-Naibu Afisa Habari na Msemaji wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania

Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania leo tarehe 22.03.2024 limeendesha zoezi la Upandaji Miti ipatayo 300 ya Matunda,Mbao na kivuli kwenye Shule ya Msingi Mwakamo na S/Sekondari Samia Mtongani zilizopo Kibaha  Vijijini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya tukio hilo la Upandaji miti Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania Mwl.Mohamed Mwampogwa alisema huu ni utaratibu tulio jiwekea Wazalendo huru kila tunapo kutana mahala tunatumia muda kidogo kupanda miti.

"Kila tunapokutana katika Vikao au Mikutano yetu au Sherehe mbalimbali za Chama au Serikali au za kitaifa kupitia Majukwaa yetu ya Wazalendo huru katika Mikoa,Wilaya,Tarafa nk huwa tunapanda miti lengo ni kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali yetu" Alisema Mwl.Mwampogwa.

"Tunaipongeza Serikali yetu kwa mapambano ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi lakini tunaiomba kupigania kupungua kwa gharama ya Gesi ili Wananchi wa hali ya chini waweze kumudu kununua Gesi kwani Matumizi ya Gesi kwa Jamii hupunguza Matumizi ya Nishati ya Kuni na Mkaa vitu ambavyo huchangia uharibifu wa Mazingira yetu" Alimalizia Mwl.Mwampogwa.

Hata hivyo tukio hilo lilihuchuliwa na Viongozi wa ngazi mbalimbali kama vile Viongozi kutoka Ofisi yá CCM Mkoa,Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Wawakilishi wa Wabunge wa Kibaha Mjini na Vijijini,Viongozi wa Tarafa,Kata pamoja na Kamati ya S/m Mwakamo.

Viongozi hao wamelishukuru Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania kwa zoezi hilo pamoja na kutoa Elimu kwa Wanafunzi wa Shule hizi mbili.Lakini pía Viongozi wa Jukwaa la Wazalendo huru ngazi ya Mkoa (Pwani) wameahidi kurudi tena kwa ajili ya zoezi la Upandaji Miti.


UZALENDO NI UTU NA UTU NI UZALENDO.




No comments