TRA kufanya kazi Jumamosi na Jumapili hii nchi nzima

 


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kwamba ofisi zake zitafanya kazi kesho Jumamosi na keshokutwa Jumapili katika ofisi zake zote nchi nzima. 

Katika Tangazo lililotolewa na Idara ya Elimu ya Mlipakodi na Mawasiliano, limewataka wafanyabiashara wote kuzitumia siku hizo kutimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kulipa kodi na kurejesha retani.

Ofisi hizo zitakuwa wazi kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi mwisho wa muda wa kazi wa kawaida.

No comments