Robinho wa Brazil akamatwa ili kutumikia kifungo kwa makosa ya ubakaji
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil Robinho amekamatwa ili kutumikia kifungo cha miaka tisa jela kwa kosa la ubakaji.
Alihukumiwa miaka miwili iliyopita nchini Italia kwa kushiriki kwake katika ubakaji wa genge dhidi ya mwanamke wa Kialbania katika klabu ya usiku huko Milan mwaka 2013.
Robinho, 40, alikamatwa nyumbani kwake katika jijini Santos.
Serikali ya Italia ilikuwa imeomba kutumikia kifungo chake nchini Brazil baada ya kushindwa kumrejesha nchini humo.
Siku ya Jumatano, mahakama nchini Brazil iliunga mkono uamuzi huo na pia iliamua kwamba anapaswa kutumikia kifungo chake jela badala ya kifungo cha nyumbani.
Mapema siku ya Alhamisi, jaji wa Mahakama ya Juu alikataa ombi la kusitisha kuzuiliwa kwake.
Hatua madhubuti iliyochukuliwa na mfumo wa haki wa Brazili imesifiwa na wengi kwenye vyombo vya habari vya ndani, ambao walihofia kwamba Robinho angekwepa adhabu kutokana na umaarufu wake na utajiri wake.
bbc

Post a Comment