Rais Museveni amteua mtoto wake kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amemteua mtoto wake, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti.
Anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya safu ya Baraza la mawaziri lililotangazwa karibuni.
Jenerali Muhoozi alikuwa akihudumu nafasi ya mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya operesheni maalumu.


Post a Comment