RC RUVUMA AKAGUA MRADI WA UJENZI BARABARA YA MATOMONDO-MLALE

 

Na Albano Midelo
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amekagua mradi wa ujenzi barabara ya Matomondo hadi JKT Mlale Halmashauri ya Wilaya ya Songea yenye urefu wa Kilometa 21 kwa kiwango cha lami nyepesi.
Kanali Abbas ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao unatekelezwa kwa awamu ambapo hadi sasa serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 5.9

Barabara hii inaunganisha kata za Mbinga Mharule na Magagura ambazo zina wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara hivyo wananchi hao wataunganishwa na barabara Kuu ya Songea-Mbambabay

No comments