Marekani yapeleka azimio UN kutaka vita Gaza isitishwe bila masharti

 

Mfadhili mkubwa wa Israel,Marekani baada ya kuona madhara kwa pande zote ya vita vya Gaza,ghafla imebadili mwelekeo na kupeleka azimio baraza la usalama la Umoja wa mataifa linalotaka vita hivyo visitishwe haraka.
Katika azimio lililopelekwa baraza hilo mwezi Februari kikwazo ilikuwa ni Marekani tu iliyopiga kura ya veto kupinga azimio hilo.

Kipengele kilichosimamiwa na Marekani wakati huo kwa kufuata misimamo ya Israel ilikuw ni kuunganishwa na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas na kwamba muda haukuwa muwafaka kwa kuitaka Israel kusitisha vita kwani kungewapa ushindi Hamas.

Katika siku za karibuni misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu imemuudhi sana raisi Biden wa Marekani .Ikiunganishwa na ukatili wa kuzuia chakula na kuua ovyo kunakofanywa na Israel huenda ni miongoni mwa sababu zilizopelekea nchi hiyo kubadilisha nia yake.

No comments