Kobbie Mainoo: Kinda wa Man United ajumuishwa kwenye kikosi cha England
Kiungo wa kati wa Manchester United Kobbie Mainoo ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Uingereza kwa ajili ya mechi zijazo za kirafiki dhidi ya Brazil na Ubelgiji.
Mainoo, 18, awali aliitwa katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 lakini amepandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Gareth Southgate.
England itacheza na Brazil Jumamosi na Ubelgiji Machi 26 - zote mbili huko Wembley - mechi zao za mwisho kabla ya Southgate kutaja kikosi chake kwa Euro 2024.
Wengine wa kikosi cha wachezaji 26 waliripoti St George's Park siku ya Jumanne.
Mhitimu wa akademi ya United Mainoo amefuzu na Uingereza katika ngazi ya chini ya 17, 18 na chini ya 19.
Kijana huyo mzaliwa wa Stockport alianza mechi yake ya kwanza Manchester United dhidi ya Everton mnamo Novemba na amecheza mechi 19 zaidi.
Alifunga bao lake la kwanza kwa klabu hiyo katika ushindi wa raundi ya nne ya Kombe la FA mjini Newport mwishoni mwa Januari, kabla ya kufunga bao la ushindi dakika za lala salama dhidi ya Wolves kwenye Ligi ya Premia siku nne baadaye.
bbc

Post a Comment