JOKATE MWEGELO ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI KOREA KUSINI
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Jokate Mwegelo, atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini na kusaini kitabu cha Wageni pamoja na kusalimiana na Mhe. Balozi Togolani Edriss Mavura ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Korea kusini.
Cde. Jokate ametoa salamu za UWT pamoja na kumpongeza Balozi Mavura kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya nchini humo ikiwa ni kuendeleza mahusiano ya Kimataifa yanayohusianisha ukuaji katika sekta ya kilimo, sekta ya uchumi kwa kuwekeza katika uchumi wa bluu, uwezeshaji wa mfumo wa anwani za makazi, kuimarika kwa demokrasia, Korea kuendelea kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya kibiashara nchini n.k.
Akiwa nchini humo CDE. Jokate ameshiriki Mkutano wa 3 wa Demokrasia uliomalizika leo Machi 20, 2024 Jijini Seoul.

Post a Comment