CCM PWANI YAWASHA INDIKETA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI

 

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani ndg David Mramba amesema CCM imewasha indiketa baada ya kupata ushindi mnono wa uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata tatu za Fukayosi iliyoko Wilaya ya Bagamoyo, Kata ya Mlanzi iliyoko Wilaya ya Kibiti na Kata ya Msangani iliyoko Wilaya ya Kibaha Mjini huku ikiwaacha midomo wazi Vyama Pinzani vilivyoshiriki uchaguzi huo.


 Ndg. Mramba amesema Wananchi wa Mkoa wa Pwani wameonyesha Upendo Mkubwa kwa Mhe, Daktari Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa zawadi nono ya kura za kutosha kwa Wagombea wa CCM ikiwa ni kukubaliana na Kasi ya  maendeleo  inayoendelea Nchini.

Ameendelea kusema kuwa viko Vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo katika Kata ya Msangani na kujikuta vikipata mshangao baada ya CCM kushinda ni ADA - TADEA, CCK, DEMOKRASIA MAKINI, DP, N.R.A, UMD na UPDP. Katika Kata ya Mlanzi Vyama vilivyoshiriki huku vikiisindikiza CCM kushinda ni ACT - WAZALENDO, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, N.R.A, UDP, UMD na UPDP. Wakati huo Vyama vilivyoshiriki katika Kata ya Fukayosi ambapo CCM imeibuka Kinara kwa kuvigaragaza Vyama hivyo ni CCK, DEMOKRASIA MAKINI, UDP na UMD.

Aidha Ndg. Mramba amesema Wagombea wa CCM walioshinda katika Kata hizo ni Ndg. Mrisho Saidi Some wa Kata ya Fukayosi Wilaya ya Bagamoyo amepata kura  5883 Kati ya kura halali 5960 sawa na asilimia 98.7 , Ndg. Athumani Ally Mketo wa Kata ya Mlanzi Wilaya ya Kibiti amepata kura 1592 Kati ya kura halali 1732 sawa na asilimia 91.9 na Ndg.  Yohana Gunze wa Kata ya Msangani Wilaya ya Kibaha Mjini amepata Kura 5862 Kati ya kura halali 5909 sawa na asilimia 99.20. 

Katika kuhitimisha kwake Ndg Mramba amesema ushindi wa CCM ni ishara njema kuelekea kwenye chaguzi zijazo kwani wananchi Wana Imani kubwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Daktari Samia Suluhu Hassan.

Taarifa hii imeandaliwa na:

Idara ya Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM
Mkoa wa Pwani
 20/03/2024.



No comments