Waziri Kamala afariki dunia
--
Balozi Mstaafu na Waziri wa zamani wa Afrika Mashariki, Dkt. Deodorus Buberwa Kamala amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam
Dkt. Buberwa amewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi mkoa wa Kagera kuanzia mwaka 2000 hadi 2010, mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri Kamili mwaka 2008 hadi 2010
Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Uholanzi ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 aliporejea kuwa Mbunge hadi mwaka 2020.

Post a Comment