Ulaya inahitaji muongo mmoja kujenga hifadhi ya silaha, asema bosi wa kampuni ya ulinzi
Ulaya itahitaji miaka 10 kabla ya kuwa tayari kikamilifu kujilinda bosi wa kampuni kubwa ya ulinzi ya Ujerumani, Rheinmetall, aliambia BBC.
Armin Papperger alisema kuwa hifadhi za risasi kwa sasa ni "tupu".
Alitoa maoni hayo wakati wa ziara ya Kansela Olaf Scholz katika sherehe za uwekaji msingi wa kiwanda kikubwa kipya cha kutengeneza silaha huko Lower Saxony.
Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius na Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen pia walihudhuria.
Maoni hayo yanakuja siku moja baada ya maoni ya mgombea urais wa Marekani Donald Trump kuzua taharuki mpya barani Ulaya.
Mgombea huyo wa chama cha Republican alisema aliwahi kumwambia kiongozi wa dunia kwamba hatawalinda wanachama wa Nato ambao hawalipi ada zao na hata "kuwahimiza" wavamizi "kufanya chochote wanachotaka".
Rheinmetall imesema itawekeza zaidi ya $300m (£274m) katika kituo hicho kipya.Hatimaye inatarajiwa kutoa raundi 200,000 za makombora ya mizinga kila mwaka.
Bw Papperger alisema kuwa "muda mrefu" utahitajika kujiandaa dhidi ya "mchokozi anayetaka kupigana dhidi ya Nato".
"Sisi tuko sawa katika miaka mitatu, minne - lakini ili kuwa tayari, tunahitaji miaka 10," alisema.
"Lazima tutengeneze risasi [risasi] milioni 1.5 barani Ulaya," Bw Papperger aliongeza.Alisema kiasi kikubwa cha risasi za Ulaya zilitumwa Ukraine, na kuachakiasi kidogo sana katika hifadhi za Ulaya.

Post a Comment