WACHEZAJI NOBLE, BANZA, OKUTU NA KELVIN WAREJEA KIKOSINI KUJIANDAA NA AZAM FC
Wachezaji wa Nne wa Timu ya Tabora United waliokuwa wakisumbuliwa na changamoto mbalimbali wamerejea mazoezini leo kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara pamoja na michuano ya kombe la Azam Sport Federation ASFC.
Wachezaji hao ni Golikipa namba moja John Noble raia wa Nchini ya Nigeria ambaye alikuwa akisumbuliwa na malaria licha ya kucheza mechi dhidi ya Namungo iliyomalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.
Mchezaji mwingine ni Kelvin Mpemba raia wa Nchi ya Kongo ambaye alikuwa nje kwa kipindi cha miezi sita tangu alipopata majeraha kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi Singida Big Star ambapo alikuwa akipatiwa matibabu kwa kipindi chote hicho na kwamba hali yake imeimarika na hivyo tayari amejiunga na wachezaji wenzake.
“Kelvin aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya Singida Big star tangu Agosti mwaka jana ambapo alikuwa akipatiwa matibabu kutokana na jeraha lake kuwa kubwa hali iliyopelekea kuwa nje kwa kipindi cha miezi sita,baada ya kumaliza matibabu amekuwa akifanya mazoezi mepesi peke yake kwa kipindi cha wiki nne na hivyo leo hii tunamshukuru Mungu kwa urejeo wake kikosini na wenzake wamefurahi kumuona tena.
Aidha wachezaji wengine waliorejea mazoezini ni Erick Okutu raia wa Nchi ya Kongo ambaye aliumia kwenye mechi dhidi ya Namungo na kwamba afya yake imeimarika hivyo yupo tayari kwa maandalizi ya mzunguko wapili pamoja na michuano ya kombe la ASFC.
Hata hivyo mbali na Okutu mchezaji mwingine aliyerejea kikosi ni Lumiere Banza Kalumba raia wa Nchi ya Kongo ambaye alikuwa na changamoto za kifamilia jambo lililopelekea kushindwa kujiunga na Timu ilipokuwa kambini Mkoani Shinyanga Januari 17 mwaka huu na hivyo kuikosa mechi dhidi ya Simba pamoja na Namungo.
“Wachezaji wetu wamerejea baada ya kuwa nje kwa siku kadhaa, hili ni jambo zuri na tunamshukuru Mungu kwa kuwa wote sasa wana Afya njema, ukiangalia pia ujio wa Banza ndani ya Timu unakwenda kuongeza nguvu kwenye michezo yetu kutokana na uwezo aliokuwa nao na mechi ya mwisho kucheza ilikuwa ni dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.
Tabora United itashuka dimbani tena kuanza mzunguko wa pili Februali 19 mwaka huu ikimkaribisha Azam FC siku ya jumatatu kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hapa mjini Tabora na kwamba mandalizi yanakwenda vizuri chini ya kocha Mkuu Goran Copnovic.
Mwisho.
Imetolewa leo Februali 15
Na Christina Mwagala
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tabora United.

Post a Comment