Rais Dk. Samia azinadi fursa za kilimo za Tanzania kwenye Mkutano wa Mashirikiano wa Masuala ya Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya Tabianchi - Norway

 


Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongea wakati wa ushiriki wake katika Mkutano wa Mashirikiano wa Masuala ya Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika tarehe 14 Februari 2024, katika Ukumbi wa Climate House (Garden Avenue) uliopo jijini Oslo, nchini Norway.  Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) naye ameshiriki katika Mkutano huo muhimu kwa Sekta ya Kilimo. 

Aidha, Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mwana Mfalme wa Utawala wa Kifalme wa Norway, Mhe. Dkt. Seleman Jafo (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Tine Tonnes, Balozi wa Norway nchini Tanzania na Mhe. Grace Olotu, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Norway. 

Lengo la Mkutano huo lilikuwa kujadili masuala yanayohusu Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na kujadili fursa za uwekezaji katika masuala hayo.




No comments