Walinzi msafara wa Lowassa wampiga ngumi muombolezaji

 


Katika hali isiyotarajiwa, muombolezaji mmoja amepigwa ngumi na kuanguka, wakati msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Edward Lowassa akiingia jijini Arusha. Mamia ya waombolezaji walikuwa wamejipanga njiani wakimuaga kwa mara ya mwisho kiongozi huyo, lakini mmoja wa waombolezaji hao alionekana akisimama na kuinua mikono.

Ingawa haikufahamika alichokuwa akikisema wakati akisimama, muombolezaji huyo alionekana akipigwa ngumi na mlinzi na kudondoka, huku msafara huo ukiendelea.

No comments