Uwanja wa fainali Kombe la dunia 2026 watajwa
Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetangaza kuwa fainali ya Kombe la Dunia la 2026 itafanyika kwenye Uwanja wa MetLife unaomudu kubeba mashabiki 82,500 huko East Rutherford huko New Jersey mnamo Julai 19, 2026.
Ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia 2026 iliyozinduliwa siku ya jana Jumapili imebainisha kuwa michuano hiyo ambayo itashirikisha Mataifa 48 itafanyika katika miji 16 kutoka Marekani, Canada na Mexico.
FIFA imetaja viwanja vitatu vitakavyotumika kwenye mechi za waandaaji wa fainali hizo ambao ni Mexico, Canada na Marekani ambapo Mexico itaanzia Estadio Azteca huko Mexico City mnamo Juni 11, Marekani itaanzia Los Angeles Juni 12 huku Canada ikianzia Toronto Juni 12.

Post a Comment