Tajiri Mnigeria aliyepata furaha kwa watoto walemavu
Femi alijibu:
"Nimepitia hatua nne za furaha katika maisha yangu na mwishowe nilielewa maana ya furaha ya kweli."
Hatua ya Kwanza ilikuwa ni kutafuta Mali na kulimbikiza. Lakini katika hatua hii sikupata furaha niliyoihitaji.
Nikaingia hatua ya pili ya kujinunulia vitu vya thamani. Lakini niligundua kuwa vitu vyote hivi vinakupa furaha ya muda tu ambayo haidumu.
Nikaingia hatua ya tatu ya kufanya miradi mikubwa. Ni katika hatua hii nilikuwa ninasambaza 95% ya Diesel Nigeria yote na Africa Kwa ujumla. Pia nilikuwa mmiliki mkubwa wa Vessel Africa na Asia. Lakini pia hapa sikupata furaha niliyokuwa nimeifikiria.
Hatua ya nne ilikuwa ni kipindi ambacho Rafiki aliniomba kununua Wheelchairs Kwa ajili ya watoto walemavu. Walikuwa kama watoto 200 hivi.
Baada ya kuombwa na rafiki yangu nilinunua Wheelchairs 200 mara moja.
Lakini pia aliniomba niambatane naye ili nikawakabidhi watoto zile wheelchairs. Nilijiandaa nikaambatana naye.
Nikawagawia zile wheel chairs Kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona furaha ikitawala kwenye nyuso za hawa watoto. Nikawaona wamekaa kwenye wheelchairs, wakizunguka na kufurahia.
Ilikuwa ni kama wako Picnic wakisherehekea ushindi wa bahati nasibu.
NiIihisi furaha ya kweli ndani yangu. Nilipotaka kuondoka mtoto mmoja alinishika miguu yangu. Nilijaribu kujinasua taratibu lakini alinikazia macho akinitazama usoni.
Niliinama chini nikamuuliza, kuna kitu kingine unahitaji?
Jibu alilolitoa mtoto huyu sio tu kwamba lilinipa furaha bali pia lilinifanya nibadili kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Mtoto huyu alisema:
*"Ninakuangalia ili niikumbuke Sura yako, siku nikikukuta mbinguni niweze kukutambua na kukushukuru tena."*
Je Wewe mwenzangu, utakumbukwa Kwa lipi utakapoondoka kwenye hiyo Kampuni, Ofisi, Biashara, Kazini au mahali unapoishi?
Je kuna Mtu atatamani kuuona uso wako tena siku za usoni?.
Credit: EATV

Post a Comment