Serikali 'yazilegezea' Bureau De Change kupambana na uhaba wa Dola
Mkurugenzi wa utafiti wa Uchumi na sera wa BoT, Lusajo Mwankemwa amesema Taifa lina akiba ya kutosha ya dola lakini sehemu ya fedha hizo hazipo kwenye sekta rasmi hivyo kuwa ngumu kuzifikia zikihitajika.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuzipata fedha hizo. Kwa sasa Tanzania ina maduka 18 ya kubadilishia fedha yanayofanya kazi huku kukiwa na maombi mapya yanayofanyiwa kazi.
Rais wa awamu ya tano, John Magufuli aliwawekea ngumu maduka hayo akiyatuhumu kutumika kusafirisha fedha chafu ikiwemo zinazoibiwa Serikalini.

Post a Comment