RC Dar amtafsiri kivingine Profesa Janabi

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameichukulia tahadhari inayotolewa mara kwa mara na Profesa Janabi juu ya ulaji wa vyakula kwa afya ya mwili, kuwasihi wananchi kutumia fursa ya kuadimika kwa sukari kwa faida.

Chalamila amesema ukimsikiliza Dr. Janabi anasema ulaji wa sukari nyingi unasababisha maradhi mengi, kwa hiyo wakati huu ambako sukari imeadimika tuachane nayo kabisa ili usiweze kupata matatizo ya afya hapo baadaye.

Kauli hiyo ya kiongozi huyo mkubwa wa mkoa, imechukuliwa kwa hisia tofauti na wananchi waliomsikiliza, lakini wengi wakiichukulia kama utani kutokana na kawaida ya Chalamila kuongea utani hata katika wakati anaotakiwa kuwa 'siriaz'.

No comments