Chalamila: Waliojenga stendi ya mwendokasi Jangwani hawakuwa na akili, nitashangaa kama bado wanapumua

 


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezungumza hayo Februari 19. 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Temeke
Kuna Stendi ya mwendokasi pale (Jangwani), mwendokasi ile imejengwa kwenye mkondo wa maji halafu maji yakijaa pale wanaanza kulia kwamba maji yameingia kwenye magari sio kweli bali magari yameingia kwenye maji na wale wote waliotengeneza ile Stendi akili hawakuwa nazo na nitashangaa kama bado wanapumua mpaka sasa, kwa sababu hawakuangalia mabadiliko ya tabia nchi, wameleta hasara magari yale, maji yameingia kwenye yale magari lakini ukweli usiopingika ni kwamba magari ndio yaliyofuata maji, kwa hiyo ninapozungumzia watu waliofuata maji ni pamoja na vituo vya mwendokasi baadhi hufuata maji sasa kama kuna hasara wale watapaswa wapelekwe Mahakamani kwa sababu wamesababisha magari kuharibika pasipo sababu" -Chalamila


No comments