Serikali yakanusha kuzuia Tundu Lissu kuhojiwa Wasafi Radio
Serikali imesema haijatoa maelekezo yoyote kwa kituo cha redio cha Wasafi FM kuzuia mahojiano ya chombo hicho cha habari na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Tundu Lissu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Mawasiiano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kufuatia taarifa zilizosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa mahojiano hayo yameziuwa ikiwa ni maelekezo kutoka juu.
Amesema Serikali haihusiki na jambo hilo na ameitaka Wasafi Media kusema ukweli kuhusu nini kimetokea.

Post a Comment