Rais Samia awapongeza Ramadhani Brothers

 

Kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, Madame President amewapongeza vijana wawili waliopata ushindi katika shindano la Fantasy League:

"Pongezi kwa vijana wetu Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League. Safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine."

No comments