Wenye hekima wakikaa kimya wapumbavu watatawala hii dunia
Na As. Dr. Mwampogwa.
Wapo watu ambao hudanganyana kuwa kukaa kimya ni Hekima lakini huu ni mfumo wa kuwafanya watu wasiamini katika kuongea yale yanayowagusa,yale yanayojenga mtazamo na matendo mapya.
Naweza kukubali kuwa mtu mwenye Hekima anajua ni mahala au mazingira na wakati gani anapaswa kuongea na aongee nini katika jambo lililo mbele yake lakini sio kukaa kimya muda wote ndiyo ichukuliwe kama Hekima ilihali unajua usahihi wa mambo yanayoendelea.
Leo tunasoma Vitabu Vitakatifu ambavyo vimebeba Hekima ya Dunia lakini ukiangalia ni maneno yaliyonenwa na Manabii wetu pamoja Watu wa Mungu Je,wasinge yanena sisi tungeyajuaje nani vipi kukaa kimya kukawa hekima ya kufunza na kujenga Jamii yenye Ustawi bora?
Kuna kipindi hisia na mitazamo binafsi ya watu huwafunga wengine akili huku Miguu yao wakiiacha ingali ikitembea.Tunapokuwa na Nadharia ambazo tunaamini zinaweza kukomboa Jamii au kurahisisha mifumo ya maisha ya Jamii yetu yafaa kusimama nazo kwa kuzivika Nadharia hizo Vitendo halisi na sio kibaki kimya.Nadhani kuna jambo la kutafakarisha hapa "Kukaa kimya kuwa hekima"

Post a Comment